Jon Batiste
Msanii tunayemuangazia
Jon Batiste ni mmoja wa wanamuziki mahiri, aliyefanikiwa na mwenye historia yakipekee. Batiste alisoma na kupokea shahada ya kwanza na shahada ya uzamili katika masuala ya muziki kutoka chuo cha Juilliard Jijini New York. Kuanzia 2015 hadi 2022, Batiste alifanya kazi kama kiongozi wa bendi na mkurugenzi wa muziki kwenye kipindi The Late Show na Stephen Colbert kinachoruka CBS. Mwaka 2018, alichaguliwa kuwania tuzo za Grammy kwenye kipengele cha Best American Roots, na mwaka 2020 alichaguliwa tena kwenye vipengele viwili kupitia albamu yake ya CHRONOLOGY OF A DREAM: LIVE AT THE VILLAGE VANGUARD and MEDITATIONS. Mwaka 2020, alishinda tuzo ya Academy kama Best Original Score kupitia filamu Disney/Pixar -SOUL, kama sehemu ya shukrani aliwapa tuzo hiyo Trent Reznor na Atticus Ross ambao alishirikiana nao katika uandishi wa kazi hiyo. Kazi hiyo ya SOUL ilimpatia Jon tuzo nyingi ikiwemo Golden Globe, BAFTA, NAACP Image Award, na Critic Choice Award. Batiste ni mtunzi wa pili mwenye asili ya watu Weusi, baada ya nguli wa muziki wa jazz Herbie Hancock, kushinda Tuzo ya Academy katika uandishi. Albam mpya ya Batiste, WE ARE ilitoka mwaka 2021 na kupokelewa vizuri, kisha akachaguliwa mara 11 kwenye vipengele tofauti vya tuzo za Grammy, ikiwa ni mara ya kwanza kutokea kwenye historia ya Grammy. Na alishinda katika vipendele vitano ikiwemo albamu bora ya mwaka.