SERA YA VIDAKUZI YA KAMPUNI YA COCA-COLA
ILISASISHWA MWISHO: Tarehe 18 Mei 2021
Sera hii ya Vidakuzi ya Kampuni ya Coca‑Cola inafafanua aina tofauti za vidakuzi vinavyoweza kutumika kuhusiana na tovuti inayomilikiwa na kudhibitiwa nasi na ambayo umetumia kufikia Sera hii ya Vidakuzi (“Tovuti”), na jinsi unavyoweza kuvidhibiti.
Tunaweza kubadilisha Sera hii ya Vidakuzi wakati wowote. Tafadhali angalia sehemu ya “ILISASISHWA MWISHO” iliyo juu ya ukurasa huu ili kuona ni lini Sera hii ya Vidakuzi ilifanyiwa marekebisho mara ya mwisho. Mabadiliko yoyote katika Sera hii ya Vidakuzi yatatumika wakati Sera ya Vidakuzi iliyofanyiwa marekebisho itachapishwa kwenye au kupitia Tovuti.
Mipangilio ya Vidakuzi
MIPANGILIO YA VIDAKUZI UNA UDHIBITI!
Ili kujua ni vidakuzi vipi umelemaza/umezima bonyeza hapa:
Mipangilio ya Vidakuzi
Vidakuzi Muhimu - vimewashwa kila wakati
Tunatumia vidakuzi hivi kufanya mambo yafuatayo:
- Kukutambua na kukuwezesha kuingia kwenye akaunti yako ya mtumiaji;
- Kukumbuka vitendo vyako vya awali kama vile chaguo lako la idhini ya matumizi ya vidakuzi.
Maelezo ya ziada kuhusu vidakuzi hivi:
Vidakuzi vinavyohitajika hukuruhusu kutumia tovuti yetu na kutumia vipengele jinsi tunavyovitoa. Hutaweza kutumia tovuti bila vidakuzi hivi, ikiwa ni pamoja na kukuonyesha toleo na uwasilishaji wa tovuti inayolingana na muunganisho wa Mtandao unaotumia. Kwa kuongeza, vidakuzi hivi vinahakikisha kwamba unapobadilisha kurasa, unaweza kubadilisha kutoka http hadi https bila hitilafu yoyote. Idhini yako haihitajiki kwa matumizi ya vidakuzi muhimu.
Vidakuzi hivi haviwezi kulemazwa/kuzimwa kwa kutumia vipengele vyovyote kwenye tovuti hii. Msingi wetu wa kisheria wa matumizi ya vidakuzi hivi ni nia yetu halali ya kuwasilisha tovuti kwako.
Unaweza kujua zaidi kuhusu Vidakuzi vinavyotumiwa katika kituo cha mapendeleo:
Mipangilio ya Vidakuzi
Vidakuzi vya Uchanganuzi
Tunatumia vidakuzi hivi kufanya mambo yafuatayo:
- Kutazama jinsi unavyojihusisha na tovuti yetu;
- Kupata maelezo zaidi kuhusu matendo yako ya kibinafsi kati ya kurasa za tovuti yetu;
- Kuboresha tovuti yetu na kuiunda kulingana na mapendeleo yako.
Maelezo ya ziada kuhusu vidakuzi hivi:
Vidakuzi vya uchanganuzi hukusanya maelezo kuhusu jinsi wageni hutumia tovuti yetu na kuwezesha tovuti kuhifadhi maelezo ambayo tayari yametolewa (kama vile majina ya watumiaji na chaguo za lugha), ili iweze kukupa utendaji ulioboreshwa na unaofaa zaidi. Kwa mfano, tovuti inaweza kukupa taarifa muhimu zaidi za karibu nawe ikiwa inatumia kidakuzi kukumbuka eneo lako. Vidakuzi vya uchanganuzi pia hutumika kuwezesha vipengele unavyoomba kama vile kucheza video, lakini hutumika tu vinapowezeshwa na mtumiaji pekee. Vidakuzi hivi hutusaidia kukupa tovuti iliyoundwa kwa ajili ya kutumiwa kwa njia bora zaidi.
Msingi wetu wa kisheria tunapotumia Vidakuzi hivi ni kwamba umetoa idhini yako. Una haki ya kuondoa idhini yako wakati wowote. Kuondolewa kwa idhini hakutaathiri uhalali wa uchakataji kulingana na idhini kabla ya kuondolewa kwake.
Unaweza kulemaza vidakuzi hivi wakati wowote kupitia vitufe vilivyo hapa chini au kupitia mipangilio katika kivinjari chako.
Unaweza kujua zaidi kuhusu Vidakuzi vinavyotumiwa katika kituo cha mapendeleo:
Mipangilio ya Vidakuzi
Vidakuzi vya Utangazaji
Tunatumia na tunaruhusu wahusika wengine kutumia vidakuzi hivi kwa ajli ya:
- Kutoa utangazaji wa mtandaoni unaokupa taarifa muhimu;
- Kuzuia utangazaji huo kuonekana mara kwa mara.
Maelezo ya ziada kuhusu vidakuzi hivi:
Vidakuzi hivi hutumika kutoa matangazo na mawasiliano mengine ya uuzaji yanayokufaa zaidi na yanayokuvutia. Vidakuzi hivi hukumbuka kama umetembelea tovuti, na kushiriki taarifa hizi na, kwa mfano, mashirika ya utangazaji na vyombo vya habari. Kwa kuongezea, vidakuzi vya utangazaji vinaweza kutumiwa na washirika wetu kuunda wasifu wa mtumiaji, ili waweze kukuonyesha matangazo muhimu kwenye tovuti zingine na kuunda hadhira inayofanana. Pia hufanya iwezekane kupunguza idadi ya matangazo unayoonyeshwa, kwa nia ya kuzuia matangazo ya mara kwa mara ambayo yanaweza kukera mtumiaji. Msingi wetu wa kisheria tunapotumia Vidakuzi hivi ni kwamba umetoa idhini yako. Una haki ya kuondoa idhini yako wakati wowote. Kuondolewa kwa idhini hakutaathiri uhalali wa uchakataji kulingana na idhini kabla ya kuondolewa kwake. Unaweza kujua zaidi kuhusu Vidakuzi vinavyotumiwa katika kituo cha mapendeleo:
Tunatumia na tunaruhusu wahusika wengine kutumia vidakuzi hivi kwa ajli ya:
Kutoa utangazaji wa mtandaoni unaokupa taarifa muhimu;
Kuzuia utangazaji huo kuonekana mara kwa mara.
Maelezo ya ziada kuhusu vidakuzi hivi:
Vidakuzi hivi hutumika kutoa matangazo na mawasiliano mengine ya uuzaji yanayokufaa zaidi na yanayokuvutia. Vidakuzi hivi hukumbuka kama umetembelea tovuti, na kushiriki taarifa hizi na, kwa mfano, mashirika ya utangazaji na vyombo vya habari. Kwa kuongezea, vidakuzi vya utangazaji vinaweza kutumiwa na washirika wetu kuunda wasifu wa mtumiaji, ili waweze kukuonyesha matangazo muhimu kwenye tovuti zingine na kuunda hadhira inayofanana. Pia hufanya iwezekane kupunguza idadi ya matangazo unayoonyeshwa, kwa nia ya kuzuia matangazo ya mara kwa mara ambayo yanaweza kukera mtumiaji. Msingi wetu wa kisheria tunapotumia Vidakuzi hivi ni kwamba umetoa idhini yako. Una haki ya kuondoa idhini yako wakati wowote. Kuondolewa kwa idhini hakutaathiri uhalali wa uchakataji kulingana na idhini kabla ya kuondolewa kwake. Unaweza kujua zaidi kuhusu Vidakuzi vinavyotumiwa katika kituo cha mapendeleo:
Mipangilio ya Vidakuzi
Vidakuzi vya Kubinafsisha
Tunatumia na kuruhusu wahusika wengine kutumia vidakuzi hivi ili kutufaidi kwa njia zifuatazo:
- Kutoa maudhui ya midia-anuai;
- Kuweka maelezo yako salama wakati ambapo umeingia kwenye akaunti yako mtandaoni.
- Kubinafsisha matumizi yako kwenye tovuti yetu kwa kukuonyesha maudhui ambayo unaweza kuvutiwa nayo kulingana na matumizi yako ya awali mtandaoni
- Kukuonyesha matangazo machache na yaliyo muhimu zaidi kulingana na mambo yanayokuvutia
Maelezo ya ziada kuhusu vidakuzi hivi:
Vidakuzi hivi huwezesha tovuti kuhifadhi taarifa ambazo tayari zimetolewa na mtumiaji (kama vile majina ya mtumiaji na chaguo za lugha), ili iweze kukupa utendaji ulioboreshwa na unaofaa zaidi. Kwa mfano, tovuti inaweza kukupa taarifa muhimu zaidi za karibu nawe ikiwa inatumia kidakuzi kukumbuka eneo lako. Vidakuzi hivi pia hutumika kuwezesha vipengele unavyoomba kama vile kucheza video, lakini huwezeshwa tu na mtumiaji pekee. Vidakuzi hivi hutusaidia kukupa tovuti iliyoundwa kwa ajili ya kutumiwa kwa njia bora zaidi. Unaweza kulemaza vidakuzi hivi wakati wowote katika mipangilio kwenye Sera hii ya Vidakuzi au katika kivinjari chako. Vidakuzi hivi havifuatilii mienendo yako kwenye tovuti zingine.
Vidakuzi hivi hutusaidia kubinafsisha matumizi yako kwenye tovuti yetu. Kwa mfano, ikiwa unasoma makala kuhusu sukari kidogo, kwa mfano kwenye vinywaji, basi tunaweza kukuonyesha matangazo ya Coke Zero. Hii inafahamika kama matangazo ya muktadha. Ubinafsishaji wa matangazo unaweza kutegemea maelezo yaliyokusanywa kuhusu matumizi yako ya huduma zetu na data nyingine ambayo wahusika wengine wanaweza kuwa nayo kukuhusu, kama vile mambo yanayokuvutia, umri na jinsia inayobainika kulingana na data ya matumizi yako ya mtandao ambayo mtangazaji anayo kukuhusu. Tunaweza pia kutumia eneo lako la jumla kukuonyesha matangazo yanayohusiana na mahali ulipo, kwa hivyo ikiwa uko Uingereza utaona matangazo kutoka kwa watangazaji wa Uingereza. Ikiwa ungependa tovuti ikufae zaidi, tafadhali wezesha vidakuzi hivi.
Msingi wetu wa kisheria tunapotumia Vidakuzi hivi ni kwamba umetoa idhini yako. Una haki ya kuondoa idhini yako wakati wowote. Kuondolewa kwa idhini hakutaathiri uhalali wa uchakataji kulingana na idhini kabla ya kuondolewa kwake.
Unaweza kujua zaidi kuhusu Vidakuzi vinavyotumiwa katika kituo cha mapendeleo:
Mipangilio ya Vidakuzi
Uhamisho wa Kimataifa
Data yako ya kibinafsi inaweza kuhifadhiwa au kuhamishiwa katika nchi zilizo nje ya Afrika Kusini kwa madhumuni yaliyofafanuliwa katika Sera hii ya Vidakuzi. Tunapohifadhi au kuhamisha data yako ya kibinafsi nje ya nchi, tutafanya hivyo kwa mujibu wa sheria inayotumika na tutahakikisha kiwango sawa cha ulinzi kinatolewa kwa kutekeleza ulinzi ufaao. Uhamisho wa data ya kibinafsi hufanywa:
- kwa nchi inayotambuliwa na mamlaka za ndani ya nchi kwamba inatoa kiwango cha kutosha cha ulinzi; au
- kwa nchi ambayo pengine haitoi ulinzi wa kutosha lakini tunategemea ulinzi wa kimkataba tunapohamisha au kutekeleza masuluhisho mengine yanayofaa ya uhamishaji wa mpaka ili kutoa ulinzi wa kutosha.
Notisi yetu ya Faragha mtandaoni inatumika pamoja na Sera hii ya Vidakuzi. Notisi ya Faragha hukufahamisha kuhusu njia tunavyotumia, tunavyohifadhi na tunavyolinda data ya kibinafsi inayokusanywa mtandaoni. Pia hukufahamisha kuhusu haki zako za ulinzi wa data na jinsi ya kuzitumia. Tunapendekeza usome Notisi hii ya Faragha. Ikiwa una maswali au wasiwasi kuhusu Sera ya Vidakuzi au Notisi ya Faragha, unaweza kututumia barua pepe kwa dpo_africa@coca-cola.com au privacy@coca-cola.com.
Orodha ya Vidakuzi
Kidakuzi ni kipande kidogo cha data (faili ya maandishi) ambayo tovuti - inapotembelewa na mtumiaji - huuliza kivinjari chako kuhifadhi kwenye kifaa chako ili kukumbuka maelezo kukuhusu, kama vile mapendeleo yako ya lugha au maelezo unayotoa unapoingia kwenye akaunti yako. Sisi ndio tulioweka vidakuzi hivyo, ambavyo vinafahamika kama vidakuzi vya mhusika wa kwanza. Pia tunatumia vidakuzi vya wahusika wengine - ambavyo ni vidakuzi kutoka kwa kikoa tofauti na kikoa cha tovuti unayotembelea - kwa juhudi zetu za utangazaji na uuzaji. Hasa zaidi, tunatumia vidakuzi na teknolojia zingine za kufuatilia shughuli zako mtandaoni kwa madhumuni yafuatayo:
Vidakuzi Muhimu
Vidakuzi hivi vinahitajika kwa utendakazi muhimu kama vile usimamizi wa usalama wa mtandao na uwezo wa kufikia mtandao huo. Vidakuzi vya kawaida haviwezi kuzimwa.
Vidakuzi vya Uchanganuzi
Vidakuzi hivi hukusanya taarifa kama vile watumiaji wangapi wanatumia tovuti yetu au kurasa zipi ni maarufu ili kutusaidia kuboresha matumizi ya mtumiaji. Kuzima vidakuzi hivi kunamaanisha kwamba hatuwezi kukusanya taarifa ili kuboresha matumizi.
Utangazaji
Vidakuzi hivi vimewekwa na sisi na/au washirika wetu na hutusaidia kuunda rekodi ya mambo yanayokuvutia kulingana na shughuli zako za kuvinjari. Ukikubali vidakuzi hivi, utaonyeshwa matangazo ya Coca‑Cola yanayolingana na mambo yanayokuvutia unapovinjari tovuti zingine.
Vidakuzi vya Mitandao ya Kijamii
Vidakuzi hivi huwekwa na huduma mbalimbali za mitandao ya kijamii ambazo tumeongeza kwenye tovuti ili kukuwezesha kushiriki maudhui yetu na marafiki wako na vile vile mitandao yako. Vina uwezo wa kufuatilia kivinjari chako kwenye tovuti zingine na kuunda wasifu wa mambo yanayokuvutia. Hii ina uwezo wa kuathiri maudhui na ujumbe unaoona kwenye tovuti zingine unazotembelea. Iwapo hautaruhusu vidakuzi hivi, huenda usiweze kutumia au kuona zana hizi za kushiriki.