Kampuni ya Kimataifa inayojihusisha na Wenyeji

Siku ya Urithi- 24 Septemba- inatambua na kusherehekea utajiri wa kitamaduni na utofauti wa taifa letu.

24-09-2022

Ijapokuwa ilitambuliwa rasmi mwaka 1996, chanzo cha kihistoria cha siku hii kinahusiana na mazingira ambayo yanaunda taifa letu. Coca‑Cola ina imani kubwa katika uwezo wa kumbukumbu ya kihistoria. Kampuni hii iliingia katika soko la Afrika Kusini mwaka 1928, na leo tunajivunia mafanikio yetu kama kampuni ya kimataifa yenye mizizi ya kudumu humu nchini. Idadi kubwa ya watu wa Afrika Kusini wanafurahia chapa zetu za aina mbalimbali, na biashara yetu inaendelea kuwa na mchango mzuri kwa jamii za mahali tunapohudumu na kufanya kazi.

Bila shaka, Afrika Kusini ni nchi nzuri hivyo kulinda rasilimali zake ni sehemu muhimu ya kulinda urithi wake. Hivyo basi, Coca‑Cola nchini Afrika Kusini inatanguliza uendelevu katika nyanja zote za shughuli zetu za kila siku.

Mapema mwaka 2022, Coca‑Cola na washirika wake wa kuuza vinywaji walizindua JAMII, jukwaa lililounganishwa ambalo linajumuisha mipango endelevu ya Coca‑Cola. JAMII inazingatia nguzo tatu za kimkakati za udhibiti wa taka, utunzaji wa maji na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na vijana. Pia, JAMII inalenga kuvutia washirika wenye dhana sawa ili kusaidia kuongeza kasi katika matokeo ya mipango yake.

Uhifadhi wa maji ni kipaumbele cha kitaifa na hatua kubwa zimepigwa ili kuhifadhi ardhi oevu kupitia kuondoa mimea vamizi. Mapema mwaka 2022, Wakfu wa Coca‑Cola (TCCF) uliwekeza katika miradi minne mipya ili kuondoa mimea vamizi na isiyo ya kawaida ambayo hutumia mamilioni ya lita za maji kila mwaka. Miradi hii, ambayo ilipokea $987, 571 katika ufadhili wa ruzuku, itasaidia kurudisha lita za thamani kwenye mazingira na kuunga mkono uendelezaji wa mipango endelevu ya uchumi wa mzunguko.

Mipango kama hiyo iliyofanywa hapo awali na Mpango wa Kurudisha Maji nchini Afrika (RAIN) ilileta matokeo mazuri. Nchini Afrika Kusini, $1, 275M ziliwekezwa katika miradi mitano ya kurudisha maji ambayo iliondoa 3,400ha za mimea isiyo ya kawaida. Kwa kuongezea, miradi hiyo ilishirikiana na shule 100 za eneo hilo, na kuwafundisha wanafunzi kuhusu uhifadhi wa maji na usafi wa mazingira.

Pia tunajitolea kusaidia kuhifadhi eneo lingine la kihistoria linaloenziwa, Kisiwa cha Robben. Septemba mwaka huu, katika kutambua Wiki ya Usafi na Urejelezaji, umati wa watu 165, wakiwemo wanachama wa Kampuni ya Vinywaji ya Coca‑Cola Peninsula na jamii ya eneo hilo, walikusanya mifuko 750 ya takataka kutoka kwenye pwani ya Kisiwa cha Robben. Mipango kama hiyo ya usafi ilifanyika kote nchini, ambayo iliongozwa na kampuni ya Vinywaji ya Coca‑Cola ya Afrika Kusini, na kuwezesha kukusanywa maelfu ya mifuko ya takataka.

Udhibiti wa taka ni nguzo muhimu katika ajenda ya uendelevu ya Coca‑Cola. Kama sehemu ya mpango wetu wa Dunia Bila Taka, tumejidhatiti kukusanya na kurejeleza idadi sawa ya chupa au makopo tunayozalisha ifikapo 2030. Kupitia ushirikiano wetu na PETCO, kampuni ya urejelezaji plastiki (PET), tumewekeza katika mipango mbalimbali ya kukusanya na urejelezaji ili kufanikisha jitihada hii. Kupitia PETCO, tunaunga mkono zaidi ya asilimia 63 ya juhudi za kurejeleza plastiki nchini Afrika Kusini. Kupitia juhudi za 2021 za urejelezaji na kukusanya, tani 90 402 za plastiki (PET) zilizotumika zilikusanywa, na kuokoa mita 560 495 za ujazo ardhini.

Mpango mpya ni kufanya sekta ya urejelezaji kuwa ya kidijitali. Kupitia msaada wa ufadhili wa TCCF, PETCO inaongoza Project Up, ambayo inatumia BanQu, teknolojia ya blockchain. BanQu ni jukwaa la ubunifu la usimamizi wa kumbukumbu ambalo limebadilisha namna vifaa vinavyoweza kurejelezwa vinavyouzwa, kufuatiliwa na kupatikana. Kutokana na hayo, kwa mara ya kwanza, Afrika Kusini inaunda kumbukumbu za kidijitali za kitaifa za vitu vinavyoweza kurejelezwa.

Coca‑Cola nchini Afrika Kusini inaendelea kuhamasisha utengenezaji wa ajira katika taratibu zetu za kuongeza thamani ya bidhaa, kuanzia ununuzi wa viambato vilivyotengenezwa ndani ya nchi hadi kuwasaidia wateja wanaouza vinywaji vyetu. Pamoja na washirika wetu wanaofanya biashara ya vinywaji, Mfumo wa Coca‑Cola (kama unavyojulikana) huajiri moja kwa moja takriban watu 10,000. Aidha, Mfumo huu huchangia maendeleo ya kiuchumi ya jamii humu nchini kupitia kodi inayotozwa Coca‑Cola inaponunua bidhaa, huduma, na vifaa vya mtaji kutoka kwa wauzaji wa humu nchini, na hivyo basi kuanzisha mipango endelevu katika ijamii.

Tunaendelea kuwekeza katika ukuzaji wa chapa za humu nchini. Chapa kama vile Stoney, Appletiser na Grapetiser hupata msaada mkubwa wa uwekezaji wa masoko na usambazaji. Kutokana na jitihada hizo, wao ni mifano inayojulikana na inayopendwa katika nyumba nyingi nchini.

Mwaka huu, Coca‑Cola nchini Afrika Kusini, kampuni ya kimataifa inayojitambulisha na Wenyeji wa Afrika Kusini, inajivunia alama mashuhuri ya miaka 94 ya kuwaburudisha wateja wa Afrika Kusini.