Coca‑Cola inaendelea kukua na kuwa kampuni ya vinywaji baridi

Usemi, "Mabadiliko tu ndio hudumu", ni kweli.

21-10-2022

Miaka ya 2010 ilikuwa miaka ya uvumbuzi na mabadiliko ya haraka, ikiongozwa na mabadiliko ya kidijitali na maendeleo katika teknolojia, ambayo iliharakisha ukuaji wa akili bandia (AI), biashara ya mtandaoni, mitandao ya kijamii, na teknolojia ya kibayolojia. Pia tabia za ununuzi zilibadilika, watumiaji walipozidi kuwezeshwa kuhusu mapendeleo yao na walipoweza kuzungumza zaidi kuhusu matarajio yao ya uwazi na maadili ambayo ambapo waliziwajibisha biashara. 

"Kwa Coca‐Cola, kusikiliza watumiaji wetu na kukubali mabadiliko ni sehemu muhimu ya kuwepo kwetu na pia ni mkakati wetu wa ukuaji. Kwa sababu hizi, tunaendelea kubadilika kuwa kampuni kamili yenye vinywaji mablimbali kwa kubadilisha mkakati wetu wa ukuaji na mtindo wa uendeshaji kulingana na mabadiliko ya ladha ya watumiaji na tabia za ununuzi, "anasema Phillipine Mtikitiki, Makamu wa Rais wa Biashara ya Coca‑Cola Afrika Kusini.

Coca‐Cola ya kwanza iliuzwa katikati mwa jiji la Atlanta mwaka 1886. Katika mwaka wa kwanza, iliuza vinywaji tisa pekee kwa siku. Sasa hivi, miaka 136 baadaye, tuna bidhaa zaidi ya 200 duniani kote, katika makundi mbalimbali na vinywaji vyetu vinatumiwa kila siku duniani kote. 

Vipaumbele vya biashara vya Coca‑Cola vitahakikisha kuwa tunaboresha mawanda ya bidhaa zetu, kutoa vifungashio vidogo, na kuwapa watumiaji taarifa ya wazi ya lishe. Tunawekeza kwenye bidhaa zenye manufaa zaidi na tutaendelea kuzalisha vinywaji vinavyoongoza kwenye sekta hii katika kategoria mbalimbali, ikijumuisha bidhaa zetu za kawaida, maji, juisi, vinywaji vya michezo, kahawa na pombe nyepesi.

"Ili kuendeleza ukuaji endelevu na wenye faida, tunafanya juhudi za dhati sio tu kupanua aina ya bidhaa zetu bali kuunda bidhaa kwa njia ya makusudi," anasema Mtikitiki. 

Coca‑Cola inaunga mkono pendekezo la mamlaka kuu za afya kuhakikisha kuwa sukari kwenye vinywaji vyake ni chini ya 10% ya ulaji wa kalori ya kila siku. Sasa tuna aina mbalimbali za vinywaji visivyo na sukari na vyenye sukari kidogo. Nchini Afrika Kusini, kati ya 2016 na 2020, tumepunguza kiwango cha sukari kwa 32% katika orodha yetu ya vinywaji vilivyotiwa sukari. 

Pia tunawazia ukubwa wa vifungashio vyetu na kutoa vifungashio vikubwa kwa ajili ya sherehe za watu wengi na vifungashio vidogo, kwa matumizi ya mara moja tu. Kila kifungashio kina maelezo ya lishe ili watumiaji waweze kufanya maamuzi kuhusu kile wanachokunywa na kufurahia vinywaji vyetu kwa ukubwa wanaotaka. Tunaongoza kwa mfano na tunajumuisha katika utangazaji wetu vinywaji vyetu baridi na visivyo na sukari kama vile Coca‑Cola Light na Coca‑Cola No Sugar.

Tunajivunia kuwa kampuni ya kimataifa yenye mizizi humu nchini. Tangu 1928, tumeshiriki katika matukio makubwa zaidi ya Afrika Kusini na kuchukua jukumu muhimu katika kukuza uchumi na kusaidia biashara za humu nchini. Tunaendelea kuchochea kutengeneza nafasi za ajira katika taratibu zetu za kuzalisha bidhaa kwa kununua viambato vya hali ya juu vilivyozalishwa humu nchini na kuwapa wateja wanaouza vinywaji vyetu ujuzi wa biashara. 

Pamoja na washirika wetu wa kuuza vinywaji, tunafanya kazi kwa karibu na wadau, ikiwa ni pamoja na serikali, jamii za ndani, na washirika wa sekta hii, kuhakikisha kwamba tunaleta manufaa kwa jamii za maeneo ambapo tunafanya biashara. Kwa kuongezea, mfumo wa Coca‑Cola - sisi wenyewe na washirika wetu wa kuuza vinywaji - huchangia maendeleo ya kiuchumi ya jamii za ndani kupitia kodi, kwa kununua bidhaa, huduma na vifaa vya mtaji kutoka kwa wauzaji wa ndani na kuanzisha mipango ya maendeleo ya kijamii.

Kama Benjamin Franklin alivyosema, ""Mabadiliko tu ndio hudumu katika maisha. Uwezo wa mtu wa kukabiliana na mabadiliko hayo utaamua mafanikio yake. Coca‐Cola itaendelea kuboresha chapa zake, kwa kutengeneza bidhaa zinazopendwa na watu na kujenga mustakabali endelevu wa biashara yetu, Afrika Kusini na ulimwenguni. Tunafanya yote haya huku tukisalia waaminifu kwa lengo letu la: Kuburudisha Ulimwengu na Kuleta Utofauti.